5
1 Ninawasihi wazee waliomo miongoni mwenu, mimi, niliye mzee mwenzao na shahidi wa mateso ya Kristo, na ambaye vile vile ni mshirika katika utukufu utakaodhihirika.
2 Kwa hiyo, ninawatia moyo ninyi wazee, lichungeni kundi la Mungu lililo miongoni mwenu. Liangalieni, sio kwa sababu mnapaswa, lakini kwa sababu mnatamani hivyo, kulingana na Mungu. Liaangalieni, sio kwa kupenda pesa za aibu, lakini kwa kupenda.
3 Msijifanye mabwana juu ya watu waliyochini ya uangalizi wenu, lakini iweni mfano katika kundi.
4 Pale Mchungaji Mkuu atakapodhihirishwa, mtaipokea taji ya utukufu isiyopoteza uthamani wake.
5 Vilevile, nanyi vijana wadogo, nyenyekeni kwa wakubwa wenu. Ninyi nyote, uvaeni unyenyekevu na kuhudumiana ninyi kwa ninyi, kwani Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa neema wanyenyekevu.
6 Kwa hiyo nyenyekeni chini ya mkono wa Mungu uliyo hodari ili kwamba awainue kwa wakati wake.
7 Mwekeeni fadhaa zenu juu yake, kwa sababu anawajali.
8 Iweni na busara, iweni waangalifu. Yule adui yenu, ibilisi, kama simba aungurumaye ananyatia, akisaka mtu wa kumrarua.
9 Simameni kinyume chake. Kuweni na nguvu katika imani yenu. Mkijua kwamba ndugu zenu walioko ulimwenguni wanapitia mateso kama hayo.
10 Baada ya kuteseka kwa muda kitambo, Mungu wa neema yote, aliyewaita katika utukufu wa milele ndani ya Kristo, atawakamilisha, atawaimarisha na kuwatia nguvu.
11 Enzi iwe kwake milele na milele. Amina.
12 Namthamini Silwano kama ndugu mwaminifu, na nimewaandikia ninyi kwa ufupi kupitia kwake. Ninawatia moyo na ninashuhudia kwamba nilichokiandika ni neema ya kweli ya Mungu. Simameni ndani yake.
13 Waamini waliloko Babeli, waliochaguliwa pamoja nanyi, wanawasalimu, na Marko mwanangu, anawasalimu.
14 Salimianeni kila mmoja kwa busu la upendo. Na amani iwe kwenu mliondani ya Kristo.